27 Machi 2017 - 19:26
Muda wa serikali ya Al-Baghdadiy wafika mwisho nchi Iraq

Kamanda mkuu wa majeshi ya Iraq katika masambulizi ya kuikomboa Musol amesema siku ya Jumapili alipokuwa katika mkutano na waandishi wa Habari kuwa: ‘Abubakar Al-Baghdadiy’ anaidaiwa kuwa khalifa wa kikundi cha kigaidi cha Daesh, mpaka sasa amekimbia mjini wa Musol ambapo hapo ndio umekoma muda wa serikali yake nchini humo

Shirika la habari AhlulaBayt (a.s) ABNA: mmoja kati ya makamanda wakuu wa majeshi ya Iraq katika mashambulizi ya kuikomboa Musol amesisitiza kuisha muda wa utawala wa Khalifa wa kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Hayo yamesemwa na “Jeneral Abul-Amiir Yarallah”  kamanda wa mashambulizi ya majeshi ya Iraq siku ya Jumapili katika mkutano na waandishi wa habari, ambapo akitangaza habari hiyo amesema; kwa mujibu wa ripoti tuliokuwa nazo (Abubakar Al-Baghdadiy) ni muda kadhaa sasa ametoroka mji wa Musol, na hadi hivi sasa hana mawasiliano na magaidi waliopo katika mji huo.
Aidha ameongeza kusema kuwa; ripoti zetu zinaonesha kuwa (Al-Baghdadiy) amekimbilia sehemu inayoitwa Aljazirah ambayo iko karibu na mipaka wa Iraq na Syria, sehemu ambayo iko chini ya kikundi cha kigaidi Daesh.
Kamanda huyo wa Iraq ameashiria kwa kusema kuwa; siku kadhaa ziliopita kiongozi huyo wa kikundi cha kigaidi cha Daesh alijeruhiwa kufuatia mashambulizi ya anga ya majeshi ya Iraq, na kupelekwa katika mji wa Raqqeh nchini Syria kwaajili ya matibabu nchini humo.
Kamanda huyo amesema kuwa; anaedaiwa kuwa ni halifah wa Daesh, muda mrefu amepoteza nafasi yake baina ya magaidi hao, baada ya sehemu nyingi walizokuwa.

mwisho/290